Jumapili, Mei 11, 2014

IFAHAMU DAWA YA KUTUNISHA MISULI INAYONG'ANG'ANIWA NA IJANA WA KITANZANIA

Pengine  ni katika harakati za kuutafuta utanashati  au  ukosefu wa ajira,  na huenda ikawa ni mtindo wa kimaisha kwa vijana wengi hapa nchini na duniani kote wanaotunisha misuli. Hata hivyo wanaume walio katika harakati za kutunisha misuli au kupata maumbo yenye miraba minne, wamekuwa wakitumia dawa ili kuyapata maumbo hayo badala ya kufanya mazoezi  ya viungo.
Vijana wengi hivi sasa  wananunua kwa wingi dawa za kutunisha misuli maarufu kama ‘doping’ kwa sababu zinazotajwa kuwa ni kutafuta ajira kama vile ulinzi kwenye kumbi za starehe, ulinzi wa watu maarufu(bodyguard) na wengine mashindano ya kunyanyua vitu vizito huku wengine wakiutafuta utanashati.
Steroids
Wataalamu wa afya wanataja baadhi ya dawa zinazonunuliwa na wajenga misuli kuwa ni Anabolic Steroids, ambazo husaidia kujaza misuli na kutochoka haraka.
Ripoti  ya Wizara ya Afya na Huduma za Jamii ya Marekani inaeleza hivi: 
Dawa za steroids za kuongeza ukubwa wa misuli ni kemikali zinazohusiana na homoni za kiume (tetosterones). Dawa hizo huchochea ukuzi wa misuli na kustawi kwa maumbile ya kiume. Wavulana wanapobalehe homoni hizo huongezeka na kubadilika na hivyo kuchochea mabadiliko ambayo humfanya mvulana awe mwanamume. Nyingine ni Creatine ambazo huuzwa katika hali ya unga unga na kama ilivyo Steroids, dawa hii nayo hujenga misuli na kuondoa maumivu ya mwili na Human Growth Hormone, vichocheo ambavyo hukuza misuli ya mtu kwa wiki chache tu.
 Dawa nyingine zenye nguvu na zinazotumiwa zaidi na wanaume wanaotaka kujenga misuli ni Optimal Stack, Precision Power, Estoforce Edge, Muscle Ex Edge na Muscle Rip Edge.
Miaka ya 70, watunisha misuli wengi akiwemo Arnold Schwazenerger, walikiri kutumia Steroids kama dawa zinazowasaidia kukuza misuli yao   hata hivyo mwaka 1990,  Marekani, ilianzisha sheria ya kuzuia dawa za Steroids na kuiweka katika kundi la dawa zilizopigwa marufuku.
Uchunguzi Fichuo tz umebaini kuwa baadhi ya vijana hutumia dawa za vichocheo vya wanaume  kama testosterone kukuza misuli hiyo. Wengi hutumia dawa hizo kwa kiwango kikubwa kiasi cha mara 10 hadi 100 zaidi ya kile ambacho daktari anaweza kukuandikia.
Wengi huzipata dawa hizi nchini Afrika Kusini ambako huletwa na watu binafsi na kuzisambaza katika nyumba za mazoezi (gym) ambako vijana wengi hufanya mazoezi ya kujenga vifua.
Gosbert Msuya, mlinda mlango wa klabu ya muziki ya Maisha, anakataa kutumia dawa za kutunisha misuli, lakini anakubali kuwa wapo vijana wanaotumia dawa hizo kwa sababu mbalimbali kubwa ikiwa ni ajira na mwonekano. 
Sasa ukiwa na mwili mkubwa unapata kazi za kuwalinda watu maarufu, kulinda ‘stage’ pindi wanamuziki wanapoburudisha. Ajira nyingine ni wakati wa maadhimisho makubwa ya kitaifa, kucheza filamu, na mwonekano mzuri
anasema Msuya.
Kijana anayekunywa dawa hizi huweza kuongezeka kilo tano hadi 15 ndani ya miezi miwili. Mzunguko na msukumo  wa damu yake huongezeka kiasi cha asilimia 20, jambo linalosababisha misuli yake kujaa.
Misuli hii huonekana wazi zaidi kwani dawa hizi husaidia kuchoma kalori kwa kiasi kikubwa  n husababisha mwili  kupoteza mafuta mengi.

3 comments: