Ijumaa, Mei 09, 2014

HUU NDIO MUZIKI UTAKAOMFIKISHA BEN POL KIMATAIFA

Baada ya kurejea kutoka nchini Ujerumani, msanii wa muziki wa R&B, Ben Pol, amedai kuwa safari yake ya Ujerumani imemfanya agundue muziki utakaomfikisha Kimataifa.
Ben Pol amesema kuwa amegundua lugha sio kigezo cha kumfikisha msanii kimataifa baada ya kuona nyimbo za mataifa tofauti nchini Ujerumani zikifanya vizuri.

Kitu ambacho nime gain ni kufanya muziki ambao hauko basic na lugha
amesema Ben Pol. 
Unajua nimekuta kule kuna nyimbo za Wafaransa,Waspain ambazo zina hit kule Ujerumani lakini zimeimbwa kwa lugha za nchi tofauti. Yaani watu wameimba kwa lugha zao kama Kifaransa,Kispain,kwahiyo hiyo inamaanisha ni kwamba kwenye maisha ili utoboe ni lazima uwe na lugha lakini kwenye muziki ni mdundo. Kwahiyo hicho ni kikubwa ambacho nimejifunza kinachomfanya mtu atoboe kimataifa sio lugha peke yake na mahadhi ya muziki inaweza kuifanya nyimbo iende mbali zaidi.
Pia Ben Pol amesema safari yake pia imefanikisha kufanya video na wimbo akiwa nchini Ujerumani.
Kuna wimbo na music video nimefanya lakini nadhani ikifika wakati nitaweka wazi ni wimbo gani,vile vipande ambavyo nilikuwa naviweka ni vya kazi hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni