Mtalii mmoja muingereza amekataliwa kuingia nchini
Sri Lanka baada ya kupatikana akiwa amechorwa 'Tattoo' ya Budhaa kwenye
mkono wake.
Naomi Michelle Coleman, alikamatwa na maafisa
wakuu alipowasili katika uwanja wa ndege katika mji mkuu Colombo baada
ya maafisa wakuu kuiona 'Tattoo' hiyo kwenye mkono wake wa kulia.
Tatoo ya Naomi Michelle Coleman inaonyesha picha ya Budhaa ambaye ni Mungu waumini wa dini ya Budhaa. |
Budhaa alikuwa mtu mwenye busara na
hekima kubwa na pia mwanzilishi wa dini hiyo ambayo mafunzo yake mengi
yalijenga msingi wa dini yenyewe.
Msemaji wa polisi alisema kuwa mwanamke huyo
mwenye umri wa miaka 37, alikamatwa kwa kosa la kuwachukiza watu wa dini
ya Budhaa na pia kwa kuumiza hisia zao za kidini.
Hakimu aliamuru Bi Coleman arejeshwe nchini mwao.
Kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha wahamiaji wanaosubiri kurejeshwa makwao.
Maafisa huchukua hatua kali dhidi ya watu
wanaonekana kutusi dini ya Budhaa ambayo waumini wake wengi wanatoka
kabila la Sinhalese lenye idadi kubwa ya watu nchini humo.
Sanamu inayoabudiwa na watu wanaoabudu dini ya Bdhaa |
Bi Coleman aliwasili katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Bandaranaike siku ya Jumatatu kutoka nchini India ambapo
maafisa punde ya kuiona Tattoo hiyo ya Budhaa akiwa amekaa kwenye mauwa,
walimkamata.
Mwezi Machi mtalii mwingine muingereza, alizuiwa
kuingia katika uwanja huo baada ya maafisa kusema kuwa alijibu kijeuri
alipohojiwa kuhusu Tattoo aliyokuwa amechorwa ambayo pia ilikuwa na
Budhaa.
0 comments:
Chapisha Maoni