Baraza la Senate la Marekani limeidhinisha kwa kauli
moja mabadiliko ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa kuhusiana na
unyanyasaji wa kimapenzi katika jeshi.
Ushahidi umeimarika kuhusu visa vya unyanyasaji
wa kimapenzi katika jeshi na wito umetolewa na makundi mbalimbali kuwa
sheria mpya zibuniwe kukabiliana na dhuluma hiyo
Tatizo la ubakaji na makosa mengine
ya ngono katika jeshi limeongezeka sana hivi kwamba makao makuu ya
jeshi, Pentagon, yamefananisha matukio hayo kama saratani.
Mabadiliko yaliyoidhinishwa na Baraza la Senet
yananuia kuimarisha jinsi kesi hizi zinavyoshughulikiwa katika Mahakama
ya jeshi. Hata hivyo mabadiliko hayo lazima yaidhinishwe na Bunge la
waakilishi.
Mojawapo wa hatua hizi ni kuondoa kinga ya sasa
iliyopo ambapo mwanajeshi aliyebaka anaweza kudai kuwa yeye amefanya
kazi yake ya kijeshi kistaarabu, na kwa hivyo anapaswa kuhurumiwa hata
akipatikana na hatia.
Mabadiliko hayo yanakusudiwa kutumiwa katika kuhakikisha kuwa jeshi linawajibika.
Hata hivyo hatua hizo zimeepusha kuwatimua kazini makamanda ambao wanasimamia vitengo ambako makosa hayo yanatokea.




0 comments:
Chapisha Maoni