Jumatatu, Machi 10, 2014

HAKUNA UCHAWI ZAIDI, TUMIA UJANJA HUU KUMPATA MWANAMKE UMPENDAE

Kuna wanaume wengi wamekuwa wakikosea kutongoza.Wapo wengine labda amempenda binti fulani lakini anashindwa cha kufanya.Kuna wakati unaweza kukuta mwanaume anachokifanya anampa ofa mwanamke,mara anamwambia tukale na hata zawadi nyingine zinafuata.Jambo lililo la msingi katika maisha yetu ni kuwa wazi,mtu aelewe nini hasa unachokitaka moyoni mwako si zaidi.
Wapo ambao wanaogopa watu labda ni kwa sababu ni wazuri au wamesoma zaidi yao,lakini mapenzi ni zaidi ya hayo,unaweza kuona mtu kweli anaonekana yuko matawi ya juu jina tu,mapenzi hayana matawi ya juu wala ya chini
Ndo maana unaweza kuona mama mtu mzima na heshima zake anajisalimisha kwa kijana mdogo,au unaweza kuona mwanaume mtu mzima na hekima zake anafanya ngona na mfanyakazi wa ndani,huenda akawa mchafu au hata
si wa kutamanisha kivile.

Mapenzi ni suala pana,unaweza kujiremba ukifikiri ndo njia ya kumtamanisha mwanaume,wapo wanaume wanachokipenda sio mwanamke ajirembe.

Unaweza kuvaa kimini na nguo yenye kuonyesha sehemu kubwa ya mwili wazi,wapo wanaume wenye kuchukia hilo.

Unaweza kuvaa suruali ukifikiri ndio chaguo la wanaume,wapo ambao hawataki kusikia mwanamke anayevaa suruali.Ninachotaka kusema ni kwamba watu wametofautiana kwa namna ya mahitaji yao.

0 comments:

Chapisha Maoni