Ijumaa, Oktoba 18, 2013

MWISHO WA DUNIA 2032, KIMONDO KIKUBWA KUIPONDA DUNIA NA KUITEKETEZA...SOMA UNAJIMU HUU WA WANASAYANSI

Dunia tunayoishi, inaweza kufikia mwisho wake August 26, 2032. Kwa mujibu wa wanajimu wa Ukraine, kimondo chenye upana wa futi 1,300 kinakuja kwa uelekeo wa duniani na kinaweza kuiponda dunia kikiwa na nguvu kubwa ya nuclear.
Crimean Astrophysical Observatory wamegundua kimondo kikubwa kiitwacho 2013 TV135, weekend iliyopita na tayari jumuiya ya kimataifa ya wanasayansi imekielezea kama moja ya vimondo hatari kabisa kuwahi kugunduliwa angani.

Hata hivyo, bado, uwezekano wa kitu hicho kuiponda dunia ni mdogo na hivyo
kuna asilimia 99.9984 za maisha kuendelea kama kawaida. Kama kimondo hicho kikiikosa dunia, kina uwezekano wa kupita ndani ya maili milioni 1 za mzingo (orbit) wa sayari hiyo.
Kama 2013 TV135 ikigongana na dunia kinakadiriwa kuzalisha megatons 2,500 za mlipuko.
Hata hivyo kimondo hicho ni kidogo kuliko kitu kilichoiponda dunia na kuwaua wanyama wa zamani aina ya dinosaurs miaka milioni 65 iliyopita. Kimondo hicho kilikuwa na upanda wa maili 6.
Kimondo hicho kitakuwa kimesogea zaidi mwaka 2024, na hivyo kuwaruhusu wanasayansi kuuchambua mzingo wake na wapi kitaangukia. Hadi sasa, kimondo cha 2007 VK184 ndicho kinaaminika kuwa na nafasi ya kuiponda dunia. Kimondo hicho chenye upana wa futi 420 kitakutana na dunia mwaka 2048.

0 comments:

Chapisha Maoni