Ijumaa, Mei 19, 2017

MCHEZAJI WA SERENGETI BOYS AWATIA SHAKA CAF, APIMWA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU

Winga wa timu ya vijana wa chini ya miaka 17, Serengeti Boys, Abdul Suleiman aliyeibuka mchezaji bora wa mechi ya Serengeti Boys na Angola hapo jana, alichukuliwa na maafisaa wa CAF kufanyiwa vipimo vya dawa za kusisimua misuli.
Hali hiyo ilisababisha ashindwe kwenda kupokea tuzo yake ya mchezaji bora hivyo akawakilishwa na mlinzi, Dickson Job. CAF hawakuamini walichokiona kwa Abdul ambaye alihaha uwanja mzima!
Hata hivyo baada ya vipimo ilibainika hakuwa katumia dawa hizo bali ni uwezo binafsi wa mchezaji uwanjani.

0 comments:

Chapisha Maoni