Kijana mmoja mkazi wa kijiji cha Nyambogo wilayani Rorya mkoani Mara,
ambaye anadaiwa kupotea nyumbani kwa imani za kishirikina hatimaye
amepatikana huku akiwa katika hali ya kutisha bila kujitambua na mwili
wake ukiwa umejaa tope jingi, tukio ambalo limevuta mamia ya wananchi wa
kijiji hicho.
kijana huyo Kenedy oguko mwenye umri wa miaka 22
amekutwa nje ya nyumba yao asubuhi ya Juni tano mwaka huku,akiwa uchi wa
mnyama,ambapo baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa
tangu kutoweka kwa kijana huyo siku nne zilizopita,wamekuwa wakimtafuta
bila mafanikio huku wakihusisha tukio hilo limefanywa kwa imani za
kishirikina.
kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya
Rorya Bw Samwel Kiboye,ambaye ni miongoni mwa mashuhuda wa tukio
hilo,amewaomba wananchi kuacha kulipiza visasi kwa kuwasaka watu
wanaotuhumiwa kwa ushirikina bali watumie vyombo vya dola huku
mwenyekiti wa kijiji hicho akilaani vikali vitendo hivyo vya ushirikina
vinavyoendelea kijijini hapo hatua ambayo amesema imesabisha wananchi
sasa kuishi kwa hofu kubwa.
hata hivyo katika hali ya kushangaza wazee wa jadi
kijijini hapo waliagiza kila mwananchi kupita mbele ya kijana huyo na
kumpa mkono kama njia moja wapo ya kuwezesha kupata fahamu kitendo
ambacho hata hivyo hakikuzaa matunda.
0 comments:
Chapisha Maoni