MSANII wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha
ambaye kwa sasa yuko Kenya amesema kuwa, haamini kama kweli wasanii wa
filamu Recho Haule na Adam Kuambiana wamefariki dunia mpaka siku
atakapoyaona makaburi yao.
Madaha alisema ameshitushwa na vifo hivyo na vimemfanya akose amani
kutokana na namna walivyoondoka duniani ghafla.
Nilitamani sana kuwepo lakini niko mpakani mwa Kenya na Uganda kuna ziara maalum ya kikazi naifanya.Yaani bado siamini kama kweli wamefariki, mpaka nije nione walipozikwa
alisema Baby Madaha.
0 comments:
Chapisha Maoni