Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Yanga na Mbeya
City lililofanyika jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam limeingiza sh. 175,285,000.
Watazamaji 30,411 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio
sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Yanga ndiyo iliyoibuka
na ushindi wa bao 1-0.
Mgawanyo wa mapato ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh.
26,738,389.83, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,919,200 wakati kila klabu
ilipata sh. 42,960,086.50.
Uwanja sh. 21,844,111.53, gharama za mechi sh. 13,106,466.92, Bodi ya
Ligi sh. 13,106,466.92, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
6,553,233.46 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 5,096,959.36.
Nayo mechi ya Simba na Oljoro JKT iliyochezwa Februari 1 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 47,705,000 ambapo
kila timu imepata sh. 11,254,122 kutokana na watazamaji 8,267.
Mgawanyo mwingine katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Simba kushinda
mabao 4-0 ni Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 7,277,033.90 na
gharama za kuchapa tiketi sh. 2,278,400.
Uwanja sh. 5,722,434.92, gharama za mechi sh. 3,433,460.95, Bodi ya
Ligi sh. 3,433,460.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
1,716,730.47 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 1,335,234.81.
0 comments:
Chapisha Maoni