Julia baraza ambaye alikuwa amevalia kisibao
,ukanda wa manjano na viatu vyenye kisigino kirefu alishangazwa na
sheria hizo mpya ambazo zilimsababisha kukosa misa ya asaubuhi.
Kulingana
na gazeti la the standard nchini kenya,Julia alisema kuwa watu wawili
walimsimamisha nje ya mlango wa kanisa hilo na kumwambia kwamba mtindo
wake wa mavazi ulipigwa marufuku katika kanisa hilo na kwamba ametakiwa
kuvaa mavazi ya heshima.
Aidha wasichana waliokuwa wamevalia suruali walilazimishwa kujifunga leso juu yake.
Julia alisema kwamba iwapo makanisa yataanza kufuata sheria kama hizo basi wengi hawatahudhuria maombi.
Baadhi
ya waumini wamesema kuwa mhubiri wa kanisa hilo aliyejulikana kama
Joseph pekee alikuwa ametangaza katika ibada ya awali kwamba mavazi
yasio ya heshima hayatakubalika katika kanisa hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni