Mauaji ya kutumia silaha nchini Marekani ni mara 25 zaidi kuliko nchi nyigine zilizostawi duniani.
Uchunguzi uliofanywa na Chuo Kikuu cha Nevada-Reno na Kitivo cha Afya ya Umma cha Harvard T.H unaonesha kuwa, uwezekano wa Mmarekani kuuliwa kwa silaha ni mara 10 zaidi ikilinganishwa na katika nchi 22 zenye kipato cha juu. Takwimu hizo pia zinaonesha kuwa, mauaji ya watu ni sababu ya pili ya vifo vingi zaidi kati ya Wamarekani wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24.
Erin Grinshteyn, mhadhiri wa Kitivo cha Afya ya Umma cha Chuo Kikuu cha Nevada ambaye ameongoza uchunguzi huo amesema zaidi ya thuluthi mbili ya mauaji nchini Marekani yanafanyika kwa kutimia silaha moto. Utafiti huo pia unaonesha kuwa, kiwango cha kujiua kwa kutumia silaha nchini Marekani ni mara 8 zaidi kuliko nchi nyingine zilizoendelea.
Zaidi ya watu elfu 33 huuliwa kila mwaka kwa kutumia silaha za moto nchini Marekani.
0 comments:
Chapisha Maoni