Maafisa wa polisi nchini Tanzania wamemtia mbaroni mshukiwa mmoja kwa kuhusiana na mauaji ya tembo wanne katika mbuga ya kitaifa ya Katavi nchini hapa.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, ameiambia Fichuo Media kuwa mshukiwa huyo kwa jina Nzuri Ndizi, kutoka kwa kijiji cha Mbede wilaya ya Mlele , Mkoa wa Katavi pia alipatikana na pembe nane ya tembo yenye uzito wa kilo 50 na yenye thamani ya dola za Marekani 60,000.
Mkuu wa polisi wa eneo hilo alisema pembe hizo zilitoka kwa tembo nne ambao waliuawa katika mbuga ya kitaifa ya Katavi.
0 comments:
Chapisha Maoni