Alhamisi, Januari 07, 2016

TAARIFA KUTOKA CECAFA

Sudan, Uganda, Zanzibar na Burundi ndio watakaokuwa wenyeji wa mashindano ya soka mwaka wa 2016, Shirikisho la soka la Afrika Mashariki na kati limetangaza.
Sudan ndiyo itakayokuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Cecafa mwaka wa 2016, huku Uganda ikipata jukumu lakuandaa michuano ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 na pia michuano ya ubingwa upande wa wanawake.
Burundi itakuwa mwenyeji wa fainali ya wachezaji wa chini ya miaka 20 na Zanzibar itakuwa na jukumu la kuwa mwenyeji wa kombe la Kagame.
Cecafa, kupitia kwa katibu mkuu, Nicholas musonye imetangaza mpango wa miaka mitano ambao uutasisitiza ukuaji wa soka ya chipukizi na wanawake pamoja na kuimarisha uwezo wa kiufundi.

0 comments:

Chapisha Maoni