Rais wa Misri, Abdel-Fattah al-Sisi, atoa ahadi ya kujenga upya makanisa yote yalioharibiwa wakati wa mashambulizi ya madhehebu, siku za nyuma.
Rais Sisi alikuwa akizungumza haya, wakati wa misa ya mkesha wa krismasi iliyokuwa imeandaliwa na wafuasi wa dini ya Coptic, mjini Cairo. Sisi akiwa amezungukwa na maskofu wa dini hiyo, aliwatakia wafuasi wote krismasi njema na kuwapongeza kwa hisia zao za kizalendo.
Hii ni mara ya pili ya kiongozi huyo kutembelea kanisa hilo, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka wa 2015.




0 comments:
Chapisha Maoni