Alhamisi, Oktoba 23, 2014

MATUKIO MAKUBWA YOTE YALIYOTOKEA MBEYA YAKO HAPA

KATIKA TUKIO LA KWANZA:

Dereva mmoja kati ya wawili ambaye hakuweza kufahamika jina wala makazi yake, jinsi ya kiume, umri kati ya miaka 25 - 30 amefariki dunia baada ya magari ya abiria waliyokuwa wakiendesha yenye namba za usajili t.473 cnt aina ya toyota hiace na gari t.135 ajf aina ya toyota hiace kugongana uso kwa uso eneo la mwisho wa waya.
Ajali hiyo imetokea mnamo tarehe 22.10.2014 majira ya saa 22:20 usiku huko maeneo ya mwisho wa waya, kata ya iyunga, tarafa ya iyunga, jiji na mkoa wa mbeya katika barabara ya mbeya/tunduma.
Aidha, watu watatu walijeruhiwa katika ajali hiyo ambao ni 1. Lameck limo 2. Angolisye mwakalobo na 3. Joyce asajile ambao wamelazwa katika hospitali ya rufaa mbeya kwa matibabu.
Chanzo cha ajali kinachunguzwa. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa mbeya.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi barakael n. Masaki anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

TAARIFA ZA MISAKO:

Katika msako wa kwanza, mtu mmoja mkazi wa mkwajuni wilaya ya chunya aliyefahamika kwa jina la prisca sinkala (31) anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa mbeya akiwa na pombe ya moshi [gongo] ujazo wa lita 05.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 22.10.2014 majira ya saa 18:00 jioni huko katika kitongoji cha majengo, kijiji na kata ya mkwajuni, tarafa ya kwimba, wilaya ya chunya, mkoa wa mbeya. Mtuhumiwa ni muuzaji wa pombe hiyo, taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea.
Katika msako wa pili, jeshi la polisi mkoa wa mbeya linamshikilia mtu mmoja aitwaye isaya daron (27) mkazi wa soweto akiwa na pombe kali [viroba] zilizopigwa marufuku aina ya boss paketi 30.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 22.10.2014 majira ya saa 14:00 mchana huko soweto, kata ya ruanda, tarafa ya iyunga, jiji na mkoa wa mbeya. Mtuhumiwa ni muuzaji wa pombe hizo.

KATIKA MSAKO WA TATU,

Mtu mmoja mkazi wa airport jijini mbeya aitwaye salehe sekile (32) anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa mbeya akiwa na kete 12 za bhangi sawa na uzito wa gramu 60.
Mtuhumiwa alikamatwa katika msako uliofanyika mnamo tarehe 22.10.2014 majira ya saa 17:30 jioni huko maeneo ya forest mpya, kata ya forest, tarafa ya iyunga, jiji na mkoa wa mbeya. Mtuhumiwa alikutwa na kete hizo baada ya kupekuliwa kwenye mifuko yake ya suruali. Aidha, mtuhumiwa ni mtumiaji na muuzaji wa bhangi hiyo.


KATIKA MSAKO WA NNE,

Jeshi la polisi mkoa wa mbeya linawashikilia watu wawili wakazi wa manga jijini mbeya ambao ni 1. Teresia mwaisakile (31) na 2. Elizabeth londele (29) wakiwa na pombe ya moshi [gongo] ujazo wa lita 01.
Watuhumiwa kwa pamoja walikamatwa katika msako uliendeshwa na jeshi la polisi mkoa wa mbeya mnamo tarehe 22.10.2014 majira ya saa 13:30 mchana huko maeneo ya manga, kata ya manga, tarafa ya iyunga, jiji na mkoa wa mbeya. Watuhumiwa ni wauzaji wa pombe hiyo, taratibu za kuwafikisha mahakamani zinaendelea.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi barakael n. Masaki anatoa wito kwa jamii kuacha kutumia dawa za kulevya/pombe ya moshi pamoja na pombe kali zilizopigwa marufuku nchini kwani ni kinyume cha sheria na ni hatari kwa afya ya mtumiaji. Aidha, anatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za mtu/watu wanaojihusisha na uingizaji/usambazaji na uuzaji wa pombe kali na pombe ya moshi ili wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

0 comments:

Chapisha Maoni